Ushughulikaji wa Wananchi ni Nini?

Ushughulikaji wa Wananchi ni mwingiliano wa pande mbili kati ya wananchi na AU ambao huwapa watu hasa sauti na utambuzi katika michakato ya kufanya maamuzi ya AU. Ushughulikaji wa wananchi unahusu umiliki, ushiriki, ujumuishaji, uwezeshaji na hatua ya kushirikiana. Unahusu kuwapa raia uwezo na jukwaa la kutatua matatizo kwa kuwa wana ufahamu na tajiriba ya kila siku ya kutoa taarifa mahususi ya muktadha ambayo huenda isiwe inapatikana kwa urahisi

Viwango vya Mwingiliano

Fahamisha

Shauriana

Ushirikiano

Uwezeshaji

  • Katika ngazi ya kwanza chini ya "fahamisha" – wananchi wanapewa taarifa sawia na sahihi ili kuwasaidia kuelewa masuala husika.

  • Katika ngazi ya pili, "shauriana"- hapa, maoni ya wananchi yanapatikana kuhusu uchambuzi au nafasi za sera za Ajenda ya 2063.

  • Ngazi ya tatu inahusiana na kuwashughulisha wananchi kama "ushirikiano". Hii ni ngazi ya juu zaidi ya kuwashughulisha wananchi ambapo wameorodheshwa kushirikiana na Umoja wa Afrika – kwa mfano, katika kubuni, utekelezaji au ufuatiliaji wa uwekezaji, miradi na mipango ya Agenda ya 2063.

  • Ngazi ya nne ya ushughulikaji ni "uwezeshaji" wa wananchi. Katika ngazi ya uwezeshaji, maamuzi ya wananchi yangekuwa ya mwisho. Hii inaweza kutekelezwa kupitia miradi ya Agenda ya 2063 iliyoundwa kuongozwa na raia na kutekelezwa na wananchi.

Sifa za Ushughulikaji

Kuwawezesha wananchi kupitia zana bunifu na vipengele shirikishi kwa ajili ya ushughulikaji wa maana

Tafiti
Shiriki maoni yako

Shiriki katika tafiti na uwe na sauti kuhusu ushughulikaji

Mapendekezo
Chapisha wazo

Uwezo wa kupenda, kutoa maoni, kufuata mapendekezo ya kila mtu na kuwa sehemu ya suluhisho kwa kuyachapisha

Hati
Shiriki maoni

Msaada wa kushirikiana kwenye hati kwa kutumia uhariri wa moja kwa moja, ufafanuzi, kutoa maoni, ukadiriaji, na uwezo wa kushiriki

Matukio
Jisajili kwa matukio

Pata nafasi ya kujisajili na ushiriki katika matukio/ mikutano

Uliza
Uliza swali

Chapisha maswali moja kwa moja kwenye ushughulikaji na upate maoni

Vikao vya Mazungumzo
Husika katika mazungumzo

Chapisha maoni kwenye ushughulikaji na ushiriki katika vikao

The Citizen Engagement Platform CEP main objective is to ensure participation of African citizens in policymaking processes through the provision of access to information as well as facilitating opportunities for interaction, exchanges and ultimately co-creation of solutions and ideas with policymakers through digital and non-digital approaches towards the attainment of Agenda 2063.

cep@nepad.org

JISAJILI KWENYE JARIDA LETU

Pokea taarifa za ajenda ya 2063

© 2025 Powered by AUDA NEPAD